MALI-MINUSMA-Ugaidi-Usalama

Mali: wanajeshi 9 wa kikosi cha Umoja wa Mataifa wauawa

Shambulio dhidi ya msafara wa magari ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma).
Shambulio dhidi ya msafara wa magari ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma). Pierre René-Worms/RFI

Wanajeshi tisa wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Niger wameuawa katika shambulizi la kigaidi liliyoendeshwa leo Ijumaa asubuhi dhidi ya msafara wa magari ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna kundi hata moja ambalo limekiri kuhusiika na shambulio hilo.

Msafara huo wa magari ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa umekua ukielekea katika eneo la Ansongo ukitokea Menaka. Wanajeshi hao kutoka Niger wamekua katika shughuli yao ya kikazi. Inasadikiwa kuwa msafara huo umeshambuliwa kwa roketi na watu wawili ambao walikua kwenye pikipiki, kama wanavyofanya mara kadhaa wanamgambo wa makundi ya kijihad.

Magari mawili pamoja na lori moja liliyokua likibeba mafuta yameteketea kwa moto baada ya kushambuliwa.Ndege za kivita na silaha nzitonzito vimetumiwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa ili kuimarisha udsalama katika eneo la tukio na kujaribu kuwasafirisha majeruhi.

Shambulio hilo limetokea karibu na kijiji cha Indelimane, hdi kwa wakati huu hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusika na kitendo hicho. Shambulio hilo limetokea kaskazini mwa Mali, katika kijiji cha Indelimane, ambacho kinajulikana kama ngome ya wapiganaji wa Mujao.

Katika tangazo liliyotolewa muda mchache baada ya kutokea tukio hilo, Serikali ya Nigeria imetoa salaam za rambi rambi kwa familia ya wanajeshi hao, huku ikiwapongeza kwa kazi nzuri waliokua wakiifanya nchini Mali.

Wakati huohuo Ofisi ya Munisma imelani kitendo hicho ikikiita kuwa ni cha unyama. Msemaji wa serikali ya Niger amesema wameanzisha uchunguzi ili kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.