BURUNDI-DRCONGO-USALAMA

Umoja wa Mataifa nchini DRCongo wathibitisha uwepo wa majeshi ya Burundi katika mji wa Kiliba

L Martin Kobler Kiongozi wa Monusco wakati alipo zuru kituo ch Kotakoli kinacho wapokea wanajeshi wanaorejea katika maisha ya kawaida
L Martin Kobler Kiongozi wa Monusco wakati alipo zuru kituo ch Kotakoli kinacho wapokea wanajeshi wanaorejea katika maisha ya kawaida Radio Okapi/John Bompengo

Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO unathibitisha uwepo wa kikosi maalum cha jeshi la Burundi mashariki mwa DRC, mjini Kiliba jimboni Kivu ya Kusini kama ilivyobainishwa na uchunguzi na Idhaa ya RFI siku za hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na RFI, Jenerali Abdallah Wafi, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC amethibitisha kuwepo kwa askari wa Burundi mjini Kiliba kwa minajili ya operesheni ya pamoja na jeshi la Congo dhidi ya waasi wa Burundi wa FNL.

Uwepo huo wa askari wa Burundi ambao kwa siku kadhaa ulitupiliwa mbali na serikali ya DRC, Umoja wa mataifa nchini DRC-MONUSCO na serikali ya Burundi hatimaye umethibitishwa kwa mara ya kwanza na ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO.

Jenerali Wafi amebainisha kuwa kwa miaka kadhaa sasa, jeshi la Burundi na jeshi la Congo FARDC wanaendesha shughuli za pamoja katika kulinda usalama wa mipaka yao, kwa kuzingatia uwepo wa waasi hao wa FNL katika Nyanda za juu tarafani Uvira.

Akitupilia mbali dhuluma zinazotekelezwa na askari hao wa Burundi dhidi ya raia wa maeneo hayo, Wafi amesema kuwa askari wa MONUSCO wanasubiri kukamilika kwa hatua ya maandalizi ya operesheni dhini ya makundi hayo yenye kumiliki silaha, kuahidi kuungana na askari wa FARDC katika operesheni ya kuwapokonya silaha, waasi wakiwemo na waasi wa FNL wa Burundi.