Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Raisi Uhuru Kenyatta ajiandaa kwenda ICC Mjini Hague, Kesi ya mauaji ya mamadou yasikilizwa huko DRC

Sauti 21:38
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Kenyagvt

Miongoni mwa habari kuu tulizokuwa nazo kwa Juma hili ni pamoja na mahakama ya kimataifa ya ICC kumtaka Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta kuhudhuria kikao kuhusu kesi yake, jumatano ya tarehe 8 mwezi huu.Na bunge maalum la katiba nchini Tanzania lilitamatisha kazi zake wiki hii mjini Dodoma, Wakati nchini DRC Kesi ya mauaji dhidi ya brigedie jenerali Mamadou Ndala Kuanza kusikilizwa mjini Beni mashariki mwa nchi hiyo.ya Rais wa Marekani Barack Obama alitumia hotuba yake katika kikao cha baraza la Umoja wa Mataifa kuomba ushirikiano wa mataifa mengine katika vita dhidi ya wapiganaji wa ISNa Katika uga wa kimataifa, Mamia kwa maelfu ya waandamanaji walimiminika barabarani huko Hong Kong nchini China kudai demokrasia , na taifa la Uturuki lilijotokeza juma hili kuungana na Marekani katika pambano lake dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu wa Islamic State na hivyo kuahidi kukabiliana na Ugaidi duniani;Ungana nami Reuben Lukumbuka, kusikiliza makala Haya,.......