RWANDA-BBC-Mauaji ya halaiki

Rwanda: Video ya BBC juu ya mauaji ya kimbari yazua utata

Katika video, rais Paul Kagame atuhumiwa kuhusika na kudungua ndege ya hayati rais  Juvénal Habyarimana.
Katika video, rais Paul Kagame atuhumiwa kuhusika na kudungua ndege ya hayati rais Juvénal Habyarimana. DR

Shirika la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka, lenye uhusiano na utawala wa Kigali limeelezea masikitiko yake kuhusu filamu iliyotengenezwa na kurushwa hewani na BBC wiki hii ambayo maudhuwi yake ni historia ya Rwanda ambayo haijawekwa wazi.

Matangazo ya kibiashara

Filamu hiyo inamtuhumu rais Paul Kagame kuhusika katika uhalifu wa kivita wa kati wa mauaji ya kimbari, mauaji ya watu wengi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mauaji ya baadhi ya wanasiasa na kuhusika na shambulio dhidi ya ndege ya hayati rais wa Rwanda, Juvénal Habyarimana.

Katika barua shirika hilo liliyomuandikia mkurugenzi mkuu wa BBC, linabaini kwamba filamu hiyo inapinga ukweli wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, huku likiomba BBC kusitisha kurusha hewani video hiyo.

“ Sisi manusura wa mauaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Watutsi nchini Rwanda, tunasikitishwa na namna kituo chenu kinadhalilisha na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya watu kutoka jamii ya watutsi ...”, barua hiyo imeanza hivo.

Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Rwanda, Kayumba Nyamwasa amemtuhumu tajiri wake wa zamani kwamba aliamuru ndege ya rais Habyarimana idunguliwe akijua kwamba mauaji dhidi ya watu kutoka jamii ya Watutsi yatatokea.

Hata hivo, wanasayansi ambao walihojiwa katika video hiyo walibaini kwamba idadi ya watu kutoka jamii ya Watutsi waliouawa iliongezwa na utawala, huku wakibaini kwamba kwa jumla ya mamilioni ya watu waliouawa mwaka 1994, wengi walikua watu kutoka jamii ya Wahutu.

Video hio imemnyooshea kidole Waziri mkuu wa zamani wa Uingerza, Tony Blair, na serikali ya Marekani, ikiwatuhumu kwamba wamekua wakimlinda rais wa Rwanda ili asifwatiliwe na vyombo vya sheria.

Akihojiwa na BBC, balozi wa Rwanda nchini Uingereza, Williams Nkurunziza ametangaza kwamba video hiyo “ imepitwa na wakati”.