Liberia: mshikamano ni silaha bora dhidi ya Ebola
Imechapishwa:
Katika mji wa Monrovia, mji mkuu wa Liberia, hata West Point, moja ya miji inayokaliwa na watu wenye maisha duni Afrika Magharibi, ni rahisi kuambukizwa virusi vya Ebola.
Ebola huathiri kila mtu. Hata mfanyabiashara wa jeneza anakabiliwa na tishio la Homa ya Ebola. Hata hivyo wakaazi wa mji wa Monrovia au West Point, wamekua wakishikama ikiwa ni moja ya silaha dhidi ya Homa ya Ebola.
Zaidi ya watu 75,000 wanaishi katika mji wa West Point, ambao unakabiliwa na Homa ya Ebola, kutokana na idadi kubwa ya watu, vile vile watu kutoka jamii mbalimbali katika mji huo wamekua wakishirikiana kwa karibu kabla na baada ya kuzuka kwa Homa hiyo. Usafi kwa raia wa mji huo ni tatizo.
Kwa sasa raia wengi wa Liberia wamekua wakishikamana kwa kuhamasishana dhidi ya Ebola hususana kuosha mikono, kutomgusa mgonjwa yeyote, kuomba msaada iwapo kunaonekana mtu mwenye dalili za virusi za Ebola,...
Mashirika mengi ya kihisani yamekua yakiwajibika kwa kupambana dhidi ya Ebola. Mashirika yanayotetea haki za binadamu na mengineyo yalisitisha shughuli zao na kwa sasa yanapambana dhidi ya Ebola.
Liberia ni miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi ambzo zinakabiliwa na Homa ya Ebola, ambayo imewaua watu zadi ya 800 na wengine wengi wamewekwa karantini.