MISRI-Usalama

Misri: Wanajeshi saba wauawa

Polisi na jeshi vyaendelea kulengwa na mashambulizi ya wapiganaji wa kiislam nchini Mirsi. Hili ni moja ya maeneo ya matukio, walikouawa wanajeshi.
Polisi na jeshi vyaendelea kulengwa na mashambulizi ya wapiganaji wa kiislam nchini Mirsi. Hili ni moja ya maeneo ya matukio, walikouawa wanajeshi. REUTERS/Asmaa Waguih

Wanajeshi saba wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika shambulio la bomu dhidi ya kifaru cha jeshi liliyotokea Jumapili jioni Oktoba 19 katika mji wa El-Arich kaskazini mwa Sinaï, nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wengine watano waliuawa katikati mwa wiki iliyopita pembezuni mwa mji wa Rafah kwenye mpaka na Gaza.

Sinaï ni moja ya maeneo ambayo yamekua yakishuhudia tangu mwezi Oktoba mashambulizi mbalimbali, baada ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kutolea wito wanajihadi wa Misri kuzidisha harakati zao dhidi ya polisi na jeshi.

Ansar Beit al-Maqdess, ni kundi lenye ushawishi mkubwa katika jimbo la Sinaï, ambalo lilitangaza hivi karibuni kuungana na Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Tangu wakati huo, zaidi ya askari polis ishirini waliuawa katika mashambulizi mbalimbali, huku mamia ya wapiganaji wa kiislam wakiuawa katika operesheni za kijeshi.

Mashambulizi mbalimbali yalitokea hivi karibuni katika miji tofauti ya Misri, ukiwemo mji kuu Cairo.