SUDANI KUSINI-TANZANIA-Mazungumzo-Mapigano-Usalama

Salva kiir na Riek Machar wanatazamiwa kukutana Arusha

Rais Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) wakikamilisha ibada kabla ya kutia saini kwenye mkataba wa kusitisha mapigano, Addis Ababa, Mei 9 mwaka 2014.
Rais Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) wakikamilisha ibada kabla ya kutia saini kwenye mkataba wa kusitisha mapigano, Addis Ababa, Mei 9 mwaka 2014. EUTERS/Goran Tomasevic (

Wajumbe maalum wa serikali za Marekani, Norway na Ujerumani, wamewataka viongozi wa Sudani Kusini Salva Kiir na mpizani wake Riek Mashar kuweka kando tofauti zao na kutafuta muafaka kwa manufaa ya taifa.

Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja wakati huu rais wa Sudani Kusini Salva Kiir na mpinzani wake Riek Mashar anaeongoza kundi la waasi, wanataraji kukutana leo Jumatatu Oktoba 20 jijini Arusha mashariki mwa Tanzania chini ya Usuluhishi wa chama tawala nchini humo CCM.

Viongozi hawa wamekutana mara kadhaa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia na kutiliana sahihi mkataba wa kusitisha mapigano na kuunda serikali ya muungano, lakini makubaliano hayo yamesalia kuwa ndoto.

Takriban watu zaidi ya laki moja wametoroka makwao na kukimbilia kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa wakihofia kupoteza maisha kutokana na swala la Ukabila, wakati huu kukiwa na hofu ya kushuhudia tena mapigano nchini Sudan Kusini.

Machafuko nchini yalioanza tangu Desemba 15 mwaka 2013 yamesababisha vifo vya mamelfu ya watu, na wengine wengi kulazimika kuyahama makaazi yao.