AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Afrika Kusini: Pistorius usiku wake wa kwanza jela

Mwanariadha wazamani mlemavu, Oscar Pistorius, ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, Oktoba 21 mwaka 2014..
Mwanariadha wazamani mlemavu, Oscar Pistorius, ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, Oktoba 21 mwaka 2014.. REUTERS/Phill Magakoe/Pool

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amelala kwa mara ya kwanza jela katika usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka uliopita.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa na Jaji Thokozile Masipa, Pistorius mwenye umri wa miaka 27 alipelekwa moja kwa moja jela kuanza kukitumikia kifungo hicho.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Masipa alisema kutokana na kosa la Pistorius kumuua mpenzi wake bila kukusudia atakitumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Mbali na kifungo hicho cha miaka mitano, Pistorius pia atakitumikia kifungo cha miaka mitatu kitakochokwenda sambamba na kile cha miaka mitano cha kumuua mpenzi wake bila kukusudia.

Familia ya Pistoris imeshtumu namna serikali ilivyoendesha kesi hiyo kwa muda mrefu, lakini ikasema imekubali hukumu ya Mahakama.

Familia ya Steenkamp imesema imefurahishwa na hukumu hiyo, huku msemaji wa Ofisi ya Mashtaka Nathi Mncube akisema Ofisi yake imesikitishwa kuwa Pistorius hakupatikana na kosa la kuua kwa kukusudia.