TUNISIA-LIBYA-Mapigano-Usalama

Tunisia: hofu ya mashambulizi mapya ya wapiganaji wa kiislam

Vikosi maalum vya Tunisia vikitumwa katika kitongoji cha Oued Ellil baada ya makabiliano ya kijeshi kati ya kundi la watu wenye silaha na polisi, Oktoba 23 mwaka 2014.
Vikosi maalum vya Tunisia vikitumwa katika kitongoji cha Oued Ellil baada ya makabiliano ya kijeshi kati ya kundi la watu wenye silaha na polisi, Oktoba 23 mwaka 2014. FETHI BELAID / AFP

Raia wa Tunisia watapiga kura Jumapili Oktoba 26 kuwachagua wabunge. Huu ni uchaguzi wa pili wa wabunge baada ya kutimuliwa Ben Ali.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa kwanza ulifanyika mwaka 2011, ambapo chama cha Ennahda kiliyo na wafuasi wengi waislamu wenye msimamo kilishinda. Mpaka sasa chama hicho kina wabunge wengi nchini Tunisia.

Katika kampeni za uchaguzi chama cha Ennahda kimekua kikikosolewa na wapinzani wake kuhusu hali ya usalama pamoja na namna kilivyo shughulikia suala la wapiganaji wa kiislam.

Hayo yanajiri wakati ambapo Alhamisi Oktoba 23 mwaka 2014, siku tatu kabla ya uchaguzi wa wabunge, makabiliano ya kijeshi kati ya kundi la watu wenye silaha na polisi yalitokea katika kitongoji kimoja cha Tunis. Viongozi wa Tunisia wana hofu kwamba huenda kukatokea mashambulizi mapya ya wapiganaji wa kiislam.

Makabiliano hayo yalitokea mapema Ahamisi asubuhi, wakati vikosi maalumu vya polisi vilikua vikijaribu kuendesha msako ndani ya nyumba moja katika kitongoji cha Oued Ellil, pembezuni mwa mji wa Tunis. Kwa mujibu wa polisi ndani ya nyumba hiyo kulikua na watu wawili wenye silaha wakiwa pamoja na wake zao na watoto, ambao walianza kuvishambulia vikosi vya usalama.

Jioni, miliyo ya risase na milipuko ya mabomu viliendelea kusikika pembezuni mwa nyumba hiyo ambayo ilikua ikizingirwa na polisi ambayo ilitumia kipazaa sauti kwa kuwataka wanawake na watoto kuondoka ndani ya nyumba hiyo.

Viongozi wa Tunisia wanahifu kwamba huenda kukatokea mashambulizi katika siku ya uchaguzi. Tunisia imekua ikishuhudia tangu mwaka wa 2013 makabiliano ya kijeshi kati ya makundi ya wapiganaji wa kiislam na vikosi vya usalama. Srikali ya Tunisia imeamua kufunga mpaka wake na libya kwa muda wa siku tatu, baada ya kuonekana kuwa wapiganaji wengi wa kiislam wanatokea Libya.

Viongozi wa Tunisia wamesema kwamba washukiwa sita ikiwa ni pamoja na wanawake watano na mwanaume moja wameuawa.