Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Hali ya wasiwasi kutanda mjini Beni mashariki mwa DRC baada ya kuwepo mauaji ya watu themanini na wanne

Imechapishwa:

Ni juma ambalo liligubikwa na simanzi kwa wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baada ya kutokea kwa mauaji ya watu themanini na wanne katika miji ya Beni na Eringeti mahsariki mwa nchi hiyo, na huko nchini Afrika kusini, jaji wa mahakama thokozile masipa alitangaza hukumu dhidi ya mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu Oscar Pistorius kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutikana na makosa ya kumuua mpenzi wake Reeva Steencamp bila kukusudia, na katika uga wa kimataifa utasikia namna ambavyo msimamo wa kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis ulizua hisia tofauti, na vile vile hali ya wasi wasi kutanda katika mji wa Kobane huko Syria, baada ya wapiganaji wa kundi la Islamic State kuukaribia mji huo.Ungana nami Reuben Lukumbuka, katika makala haya.

Sayari ya dunia
Sayari ya dunia