BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: mvutano waendelea kujitokeza kuhusu marekebiso ya Katiba

Raia wakiandamana katika mji wa Ouagadougou, Jumatano Oktoba 29 mwaka 2014. dhidi ya marekebisho ya katiba, ambayo yatapelekea Blaise Compaoré kusalia madarakani.
Raia wakiandamana katika mji wa Ouagadougou, Jumatano Oktoba 29 mwaka 2014. dhidi ya marekebisho ya katiba, ambayo yatapelekea Blaise Compaoré kusalia madarakani. REUTERS/Joe Penney

Wabunge nchini Burkina Faso wanatazamia kujadili Alhamisi Oktoba 30 muswada wa sheria juu ya marekebisho ya Katiba. Vyama vinavyounga mkono chama tawala cha rais Blaise Compaoré vinataka mabadiliko ya Ibara ya 37 ili kumpa nafasi ya kugombea kwa muhula mwengine rais Blaise Compaoré.

Matangazo ya kibiashara

Mchakato huo umeendelea kupingwa na upinzani. Iwapo muswada huo wa sheria utapitishwa kwa asilimia ndogo ya wabunge, kura ya ya maoni itaitishwa, lakini iwapo muswada huo utapitishwa kwa asilimia kubwa ya wabunge, moja kwa moja Katiba itafanyiwa marekebisho na Bunge.

Hayo yanajiri wakati ambapo mvutano ulikua ukiendelea usiku wa Jumatano Oktoba 29 kuamkia Alhamisi Oktoba 30 katika katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Mvutano umekua ukiendelea katika mji wa Ouagadougou katika mkesha wa kupitisha muswada wa sheria unaohusu marekebisho ya Katiba. Kufuatia wito uliyotolewa na vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia, vijana wengi walijaribu usiku wa kuamkia Alhamisi Oktoba 30 kuondoa vizuizi viliyowekwa na polisi mbele ya jengo la Bunge na katika maeneo ya burudani hususan eneo la taifa na kwenye randabauti ya Umoja wa Mataifa, lakini walitawanywa na polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi. Hata hivyo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika mji wa Ouagadougou, ambapo wanajeshi na waandamanaji wamekua wakinyoosheana kidole.

Lengo la vijana hao, baada ya wito wa kuandamana nchi nzima uliyotolewa Jumanne na Jumatano wiki hii, ilikua kuonyesha kuwa hawaungi mkono marekebisho ya Katiba, ambayo yatamruhusu Blaise Compaoré ambaye ni rais wa Burkina Faso tangu miaka 27 iliyopita, kusalia madarakani.