UFARANSA-MALI-BARKHANE-Ugaidi-Usalama

Mapigano kaskazini mwa Mali: mwanajeshi wa Ufaransa auawa

Vikosi maalumu vya Mali na Ufaransa katika mji wa Gao, mwaka 2012
Vikosi maalumu vya Mali na Ufaransa katika mji wa Gao, mwaka 2012 RFI/Olivier Fourt

Mwanajeshi wa Ufaransa ameuawa Jumatano Oktoba 29 kaskazini mwa Mali wakati wa operesheni ya majeshi ya Ufaransa "dhidi ya kundi la kigaidi lenye silaha" katika eneo la Adrar amesema, rais François Hollande, katika tangazo liliyotolewa na Ikulu ya Paris.

Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Jamhuri ameelezea masikitiko yake baada ya kupata taarifa mapema Alhamisi asubuhi kifo cha mwanajeshi wa Ufaransa nchini Mali, wakati wa operesheni ya majeshi ya Ufaransa dhidi ya kundi la kigaidi lenye silaha kaskazini mwa Mali", imesema Ikulu katika tangazo hilo.

Rais wa Jamhuri "ameonyesha heshima yake ya kina kwa ajili ya kujitolea ya mwanajeshi huyo wa vikosi maalum katika mpango hasa hatari ambao malengo yake yamekamilika". Rais Hollande amebaini kwamba wanajeshi wa Ufaransa wanaoshirikiana sambamba na jeshi la Mali pamoja na vikosi vya Umoja wa Mataifa, kusaidia kwa ujasiri na ufanisi ili kuimarisha usalama, kudumisha uhuru wa Mali na 'kupambana dhidi ya ugaidi".

Mapema, waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian ametangaza mbele ya wabunge kwamba "mapigano makali" yametokea usiku wa Jumanne Oktoba 28 kuamkia Jumatano Oktoba 29 kati ya kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali Barkhane na "kundi kubwa la kigaidi lenye silaha linalofananishwa na kundi la Aqmi lenye mafungamano na Al Qaeda" kaskazini mwa Mali.

Operesheni ya kutokomeza makundi ya kigaidi ilizinduliwa usiku wa Oktoba 28 hadi Oktoba 29 katika milima mikubwa ya Tigharghar. Ndege na helikopta za kivita zilitumiwa katika operesheni hiyo. Operesheni hiyo iliendeshwa karibu na ngome ya kundi moja la kigaidi. Katika eneo hilo kulitokea mapigano makali kati ya majeshi ya Ufaransa na magaidi wenye zaidi ya thelathini, mapigano ambayo yalisababisha kifo cha mwanajeshi huyo wa Ufaransa na mwengine kujeruhiwa. Mwanajeshi huyo ametimiza idadi ya wanajeshi 10 ambao wameuawa tangu majeshi ya Ufaransa yatumwe Mali kushirikiana na jeshi la nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi.