DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: watu 14 wauawa kando ya mji wa Beni

Zaidi ya watu 1500wanaishi katika shule hili la Oicha baada ya kuhofia usalama wao kutokana na mauaji dhidi yanayoendeshwa na ma kundi yenye silaha katika kijijichao katika wiaya ya Beni.
Zaidi ya watu 1500wanaishi katika shule hili la Oicha baada ya kuhofia usalama wao kutokana na mauaji dhidi yanayoendeshwa na ma kundi yenye silaha katika kijijichao katika wiaya ya Beni. RFI/LL.Westerhoff

Ziara ya rais Joseph Kabila Kabange katika mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, haikuzuiya chochote kuhusu kudorora kwa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumatano Oktoba 29 kuamkia Alhamisi Oktoba 30, watu kuni na nne waliuawa kwa kukatwa na mapanga katika kijiji cha Kampi ya Chui, kilomita 70 na mji wa Beni.

Kundi la watu wenye silaha waliendesha shambulizi katika kijiji cha Kampi ya Chui na kuwaua watu 14. Jeshi halikuingilia kati ili kulidhibi kundi hilo wakati ambapo kituo cha wanajeshi kinapatikana kwenye umbali wa kilomita 12.

Mashirika ya kiraia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamenyooshea kidole waasi wa Uganda ADF-Nalu kwamba wamehusika na mauaji hayo. Hata hivo baadhi ya vyanzo vimekua vikijiuliza kuhusu mashambulizo hayo, wakibaini kwamba bila uchunguzi ni vigumu kutuhumu kundi lolote lenye silaha.

Kiongozi wa shirika la kiraia mtaani Beni Teddy Kataliko ameliambia shirika la habari la ufaransa AFP kuwa mauaji hayo yamezusha hali ya sintofahamu kwa raia wa kijiji hicho, kwa kuwa yamefanyika wakati huu rais Joseph Kabila akizuru maeneo hayo.

Nao wabunge kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini wameiomba serikali ya DRC kuongeza jitihidi katika suala zima la uongozi wa kiserikali hali kadhalika wa kijeshi, katika kuhakikisha usalama wa wananchi unazingatiwa.