MSUMBIJI-RENAMO-FRELIMO-Uchaguzi-Siasa

Msumbiji: Filipe Nyusi achaguliwa kuwa rais

Filipe Nyusi wa chama cha Frelimo amechaguliwa raisa wa Msumbiji kwa kipindi cha miaka mitano, kulingana na matokeo ya mwisho yalitotangazwa Alhamisi Oktoba 30 mwaka 2014.
Filipe Nyusi wa chama cha Frelimo amechaguliwa raisa wa Msumbiji kwa kipindi cha miaka mitano, kulingana na matokeo ya mwisho yalitotangazwa Alhamisi Oktoba 30 mwaka 2014. Cristiana Soares/RFI

Tume ya uchaguzi nchini Msumbiji imetangaza matokeo ya uchaguzi wa urais na ubunge ulifanyika tarehe 15 Oktoba na ambapo Filipe Nyusi, mgombea wa chama cha Frelimo alichaguliwa kuwa rais kwa miaka mitano ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Filipe Nyusi ameshinda kinyanganyiro cha mwaka 2014 kwa asilmia 57.3% ambapo chama chake kitakuwa na wabunge 144 huku chama pinzani cha Renamo kikiwa na wabunge 89 na kiongozi wake Afonso Dhlakama akitangazwa kuambulia asilimia 36.61% za kura zote.

Nyusi mwenye umri wa miaka 55 atakuwa rais wa kwanza ambaye hakushiriki katika mapambano ya uhuru na ambapo ameonyesha umahiri wake akiwa mkurugenzi wa kampuni ya kitaifa ya reli kabla ya kujiunga na serikali mwaka 2008 ambapo aliwahi kuwa Waziri wa ulinzi maarufu kama mtu wa karibu wa rais anayemaliza muda wake Armando Guebuza.

Chama cha Frelimo kipo madarakani kwa miaka thelathini na tisa iliyopita na kujinyankulia ushindi katika uchaguzi wa wabunge kwa asilimia 55.97% sawa na upungufu wa wabunge47 ukilinganishwa na bunge lilioko sasa.

Chama cha upinzani cha Renamo sasa kitakuwa na wabunge 89, kikijiongezea idadi ya wabunge 38 zaidi kutoka idadi yao ya hivi sasa ya wabunge 51 na chama cha MDM kikiwa na wabunge kumi na saba tofauti na wabunge nane walioko katika bunge linalomaliza muda wake.