KENYA-POLISI-Usalama

Kenya: polisi yaandelea kulengwa na mashambulizi ya wezi wa mifugo

Polisi ya Kenya inakabiliwa na mashambulizi ya wezi wa mifugo.
Polisi ya Kenya inakabiliwa na mashambulizi ya wezi wa mifugo. Reuters

Jeshi la polisi nchini Kenya linasema limewakamata watu wawili wanaoshukiwa kuwa miongoni mwa wezi wa mifugo.

Matangazo ya kibiashara

Watu hao waliokamatwa wanatuhumiwa kwamba ni miongoni mwa wezi wa mifugo waliowaua maafisa wa polisi 21 mwishoni mwa Juma lililopita katika eneo la Turkana, wakati huu shinikizo zikiendelea kutolewa kwa Inspekta wa polisi nchini humo David Kimaiyo kujiuzulu.

Polisi nchini Kenya imekua ikilengwa na mashambulizi ya wezi wa mifugo, katika maeneo mbalimbali ya nchi.