SUDANI KUSINI-IDAD-Mazungumzo-Mapigano-Usalama

Sudani Kusini: viongozi wa Igad wawataka Kiir na Machar kukomesha mapigano

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kushoto) et lkiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) wakitamatisha maombi kabla ya kutia saini kwenye mkataba wa usitishwaji vita. Addis Ababa, Mei 9 mwaka 2014.
Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir (kushoto) et lkiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) wakitamatisha maombi kabla ya kutia saini kwenye mkataba wa usitishwaji vita. Addis Ababa, Mei 9 mwaka 2014. EUTERS/Goran Tomasevic (

Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki zinazotatua mzozo wa Sudan Kusini chini ya mwavuli wao wa IGAD, wamemtaka rais Salva Kiir na Makamu wa rais wa zamani Riek Machar kukaa chini na kuamua kusitisha mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaongozwa na Makamu wa zamani wa rais, Riek Machar yanaendelea nchini Sudani Kusini kwa mwezi wa kumi na moja sasa.

Viongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki IGAD wakiongozwa na Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalgen walikutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wamesema imedhirika wazi kuwa viongozi wa Sudan Kusini hawana hamu ya kumaliza mzozo huo ambao unaendelea kuwatesa raia wa kawaida.

Wito huu unakuja muda mfupi baada ya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi kutishia kuwawekea vikwazo viongozi wa Sudan Kusini ambao wamekuwa wakikubaliana mara kwa mara kusitisha vita bila mafanikio.

Mapigano hayo yanayoendelea kushuhudiwa nchini Sudani Kusini yamesababisha vifo vya maelfu ya raia na wengine mamia kwa maelfu waliyahama makaazi yao.