MALI-ALGERIA-WAASI-USALAMA

Mazungumzo ya amani Mali yagonga mwamba

Mazungumzo ya amani kati ya makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali na Serikali ya Bamako.
Mazungumzo ya amani kati ya makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali na Serikali ya Bamako.

Mazungumzo ya amani nchini Mali yaliyokua yakifanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers yalikamilika mwishoni mwa wiki iliyopita. Mazungumzo ambayo yalikua katika duru ya mwisho hayakuruhusu makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali na viongozi wa Mali kufikia mkataba.  

Matangazo ya kibiashara

Mvutano ulijitokeza katika kikao hicho ambacho kilikua kilipangwa kua cha mwisho katika mazungumzo yaliyokua yakiwashirikisha wajumbe wa makundi yenye silaha na wale wa serikali ilikufikia mkataba wa amani ya kudumu. Kikao kingine kinatazamiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2015.

Mazungumzo kati ya makundi hayo yenye silaha na serikali ya Mali yaliyokua yakifanyika mjini Algiers yangelifanyika kulingana na rasimu ya mkataba iliyoandikwa na Jumuiya ya Kimataifa ambayo inasimamia usuluhishi katika mazungumzo hayo. Lakini wakati wa ufunguzi wa kikao hiki, makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali yaliwasili mjini Algiers yakiwa na rasimu yao ya jinsi taifa la Mali linapaswa kuogozwa, rasimu ambayo hawataki kuitupilia. Mohamed Ousmane Ag Mohamedoun, mfuasi wa kundi lenye silaha la CPA linaloendesha harakati zake katika maeneo ya Azawad, amesema rasimu waliyoandaa hawawezi kuitupilia, kwani ina mambo mengi ambayo yatachangia kuleta amani ya kudumu Mali.

" Changamoto ziliyopo kufuatia miaka kadhaa iliyopita katika suala la kuchelewa katika utawala bora na katika maendeleo. Baada ya miaka 50, tunaamini kwamba ni mfumo ambao hauwajibiki. Ni mfumo mwengine mpya ambao unaweza kuwa suluhisho katika uhusiano na ikilinganishwa na jimbo hili ili kujazia pengo linalozikabili sekta hizo”, amesema Mohamed Ousmane Ag Mohamedoun

Lakini katika mkutano huo, wawakilishi wa serikali walighadhibishwa na baadae kukataa kuongezwa muda wa mazungumzo kutokana na jinsi rasimu hiyo iliyoandaliwa na makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali ilichukua muda mrefu kwa kuisoma.

Kwa upande wake Abdoulaye Diop, waziri wa mambo ya kigeni wa Mali, "mazungumzo haya yanapaswa kufuata muongozo wa upatanishi, lakini tunachoshuhudia hapa ni kwamba tumeletewa rasimu ambayo inakuja kutupotezea muda, wakati ilipingwa majuma kadhaa yaliyopita na Jumuiya ya Kimataifa iliipinga .