MALI-ALGERIA-WAASI-USALAMA

Viongozi wa Mali washindwa kuzungumzia kufeli kwa mazungumzo

Wawakilishi wa serikali ya Mali na wawakilishi wa makundi yenye silaha wakikutana katika mazungumzo katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.
Wawakilishi wa serikali ya Mali na wawakilishi wa makundi yenye silaha wakikutana katika mazungumzo katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE

Awamu ya mwisho ya mazungumzo kati ya Bamako na makundi ya waasi kaskazini mwa Mali yalifanyika wiki iliyopita katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. Mvutano kati ya pande hizo mbili ulipelekea kushindwa kuandaa rasimu ya mkataba.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe katika mazungumzo walirejea nyumbani wakiwa na pendekezo la nakala ya timu ya upatanishi. Jumanne Desemba 2, mawaziri kadhaa wa Mali walipowasili mjini Bamako wamezungmza mbele ya vyombo vya habari ambapo walijaribu kueleza kwamba kulikuwa hakuna mvutano katika mazungumzo hayo.

Mawaziri hao wamebaini kwamba katika mazungumzo hayo kulijitokeza tu hali ya kuhitilafiana katika baadhi ya mambo wala hakuna mvutano wowote uliyojitokeza.

Kama mawaziri wa Mali walieleza walipowasili Bamako kwamba awali mazungumzo yaligubikwa na hali ya kuhitilafiana kati ya pande mbili husika, walitaka kusiwepo na sababu za kuzusha chokochoko au uhasama.

Ousmane Sy, Waziri wa mambo ya ndani, ameelezea tukio ambalo amesema linapaswa kupongezwa, wakati mkutano ulipomalizika, wawakilishi wa serikali ya Mali walipeana mikono na wawakilishi wa makundi yenye silaha, huku wakila chakula cha mchana na jioni wakiwa pamoja.

" Isahara hiyo inaonesha nini? Ishara hiyo inaonesha kuwa kulikua hakuna uadui au mvutano wowote kati yetu", amesema Ousmane Sy.

Mawaziri hao wa Mali wamehakikisha kuwa hatua imepigwa katika mazungumzo hayo hata kama wamekubali kwamba pendekezo jipya waliloopewa na timu ya upatanishi inafanana kwa sehemu kubwa na lile lililotolewa awali. Nakala hiyo ilioyopendekezwa na timu ya upatanishi itasaidia kufikia mkataba wa mwisho.