ZIMBABWE-MUJURU-MUGABE-SIASA

Mugabe amteua Waziri wa sheria kuwa mrithi wake

Waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, ateuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF na Makamu wa rais wa Zimbabwe, Desemba 10 mwaka 2014.
Waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, ateuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF na Makamu wa rais wa Zimbabwe, Desemba 10 mwaka 2014. REUTERS/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemteua waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, kuwa mrithi wake.  

Matangazo ya kibiashara

Emmerson Mnangagwa, ameteuliwa Jumatano Desemba 10 mwaka 2014 kuwa naibu mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF, na makamu wa rais wa taifa la Zimbabwe. Nafasi hiyo ni mhimu, wakati ambapo rais Mugabe ana umri wa miaka 90.

Iwapo kifo kitamkuta Robert Mugabe hakuna shaka, mrithi wake ndio atapaswa kuchukua madaraka ya uongozi wa nchi.

Emmerson Mnangagwa, ni mshirika wa karibu wa Robert Mugabe. Aliwahi kuhudumu kwenye wizara muhimu. Aliwahi kuwa Waziri wa Usalama wa taifa, Waziri wa ulinzi na Waziri wa sheria.

Emmerson Mnangagwa ni mtu anayeogopwa. Aliwahi kukomesha machafuko ya watu waliokua walijitenga katika majimbo ya Matabeleland na Midlands baada ya uhuru. machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu 20, 000. Mnangagwa alijua baadaye kuwa alifundishwa " kuharibu na kuua" kabla.

Huenda akawa mmoja kati ya watu tajiri katika utawala wa Mugabe, akipata faida hususan katika miogodi ya dhahabu.

Kulingana na mwanadiplomasia mmoja wa Marekani, kiongozi huyo alipata utajiri, kufuatia dhahabu alizo kua akijizolea wakati alipomsaidia rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent Kabila, kupambana na waasi nchini humo.

Miezi ya hivi karibuni, Mnangagwa, alishirikiana na mke wa Robert Mugabe, Grace Mugabe, ili wamuangushe Joice Mujuru kwenye wadhifa wa Waziri mkuu tangu miaka kumi iliyopita. Mujuru alifutwa kazi mwanzoni mwa juma hili. Mnangagwa kwa sasa ni mrithi wa Robert Mugabe.