MAURITIUS-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani washinda kwa kishindo

Sir Anerood Jugnauth, mwenye umri ya miaka 84, aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Mauritius, tangu mwaka 1983 hadi 1995.
Sir Anerood Jugnauth, mwenye umri ya miaka 84, aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Mauritius, tangu mwaka 1983 hadi 1995. DR

Upinzani nchini Mauritius, ukiongozwa na Sir Anerood Jugnauth, umejinyakulia idadi kubwa ya viti Bungeni.  

Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura nchini Mauritius wamekaribisha na kupongeza muungano wa mkongwe huyo katika siasa, ambaye aliwahi kuwa Waziri mkuu tanguya mwaka 1983 hadi 1995.

Muungano unaoongozwa na Sir Anerood Jugnauth, mwenye umri wa miaka 84, umepata viti 47 kwa jumla ya viti 60 Bungeni. Sir Anerood Jugnauth, amemshinda mshindani wake Navin Ramgoolam, anaye maliza muda wake, ambaye chama chake kimepata viti 13 pekee.

Navin Ramgoolam hakuweza kuokoa chama chake, hata wadhifa wake ameupoteza. Waziri Mkuu anayemaliza muda wake ambaye pia ni kiongozi wa chama kiliyotawala kwa kipindi kirefu nchini Mauritius ameshindwa pia katika eneo linalokaliwa na wafusi wengi wa chama chake, ambapo muungano unaoongozwa na Jugnauth umepata kura nyingi. Hata hivyo, awali, Ramgoolan na mshirika wake Paul Beranger walitabiriwa kuwa watashinda viti vyote 60 bungeni, jambo ambalo halikuwezekana.

Sir Anerood Jugnauth ametangaza kuunda serikali haraka iwezekanavyo. Ameahidi kuwa angeweza kufanya kazi kufikia kiwango cha juu katika sekta ya uchumi, ambacho kinakumbusha miaka ya ajira wakati wa utawala wake katika miaka ya 1983 hadi 1995.