BURUNDI-UPINZANI-CENI-UTAWALA-SIASA-USALAMA

Wanasiasa Burundi wakubaliana

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Novemba 4 mwaka 2014.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Novemba 4 mwaka 2014. AFP PHOTO/JENNIFER BRUCE

Mkutano kuhusu kujadili namna zoezi la kujiorodhesha lilivyoendeshwa uliyofanyika Jumatatu Desemba 22 mwaka 2014, umepelekea upinzani na vyama vya kiraia kuwa na matumaini ya uchaguzi wa mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulikua umeandaliwa na tume huru ya uchaguzi (Céni) kwa niaba ya wadau wote katika mchakato wa uchaguzi, hususan wanasiasa na mashirika ya kiraia.

Mchakato wa uchaguzi ulikuwa katika hatihati ya mlipuko kutokana na udanganyifu mkubwa kufuatia usambazaji kiholela wa vitambulisho vya uraia vilivyotumiwa katika zoezi la kuandika wapiga kura lililomalizika Ijumaa, Desemba 19.

Vyama vya kiraia vimekua vikiomba kufutwa kabisa kwa matokeo ya zoezi hilo la uandikishaji, huku upinzani ukiungana kwa pamoja na kuomba tume huru kujiuzulu haraka iwezekanavyo bila masharti.

Lakini tume hii ya uchaguzi imeweza kupunguza mvutano uliyokua ukishuhudiwa kwa kuleta maelewano, jambo ambalo, limekaribishwa na jumuiya ya kimataifa na vyama vya kiraia.

Kwa muda wa saa nane za mjadala, tume huru ya uchaguzi imeeleza kuwa kulingana na sheria ya uchaguzi wakati kunakojitokeza kasoro aidha udanganyifu katika zoezi la kuandika wapiga kura, kunahitajika utaratibu fulani hususan kuchunguza orodha ya waliojiandikisha, kufuta watu waliyojiandikisha zaidi ya mara moja au kupiga marufu mtu kupiga kura zaidi ya mara moja.

“ Lakini njia zote hizo zinaonekana kuwa hazitoshi”, amesema Pierre-Claver Ndayicariye, mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi (Céni).

Pierre-Claver Ndayicariye amesema atapendekeza zoezi la kuandika wa piga kura lirejelewe katika baadhi ya maeneo ili kuruhusu wafuasi wa upinzani ambao hawakujiorodhesha, waweze kujiorodhesha.

Pierre-Claver Ndayicariye amesema pia kuwa watafu utaratibu wa mtu kupiga kura zaidi ya mara moja katika chaguzi za mwaka 2015.

Hata hivyo vyma vya upinzani vimeendelea kuomba kufanyike mkutano mwengine wa kutathmini zoezi la kujiorodhesha kwa wapiga kura nchini Burundi, ambao hautaongozwa na CENI.