COTE D'IVOIRE-SIMONE-ICC-SHERIA

Kesi ya Simone Gbagbo yaanza kusikilizwa Abidjan

Kwa mujibu wa wanasheria wake, Simone Gbagbo anasubiri kuripoti mbele ya majaji ili kujua anachotuhumiwa.
Kwa mujibu wa wanasheria wake, Simone Gbagbo anasubiri kuripoti mbele ya majaji ili kujua anachotuhumiwa. 1.bp.blogspot.com

Kesi ya Simone Gbagbo, mkee wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo pamoja na watuhumiwa wenzake 82 walioshikilia nyadhifa mbalimbali katika utawala wa rais huyo itaanza kusikilizwa leo Ijumaa Desemba 26.

Matangazo ya kibiashara

Simone Gbagbo na watuhumiwa  wenzake 82 wanakabiliwa na mashitaka ya kuhatarisha usalama wa taifa. Ni kesi ya kwanza baada ya machafuko yaliyotokea mwaka 2010 inayojumuisha raia wasiokua wanajeshi walioshikilia nyadhifa mbalimbali katika utawala wa Laurent Gbagbo kuanza kusikilizwa. Watu hao wanatuhumiwa kwa uhalifu uliyotekelezwa baada ya uchaguzi uliyofanyka mwaka 2010.

Watuhumiwa hao watasikilizwa chini ya ulinzi mkali kwa mara ya kwanza na majaji, lakini raia hawatapewa nafasi ya kusikiliza kesi hiyo, kwani bado haijawekwa katika hatua ya kusikilizwa hadharani.

Kesi hiyo imecheleweshwa kwa kipindi cha miezi miwili ikilinganishwa na muda uliyokuwa ulipangwa ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Simone Gbagbo amekua sasa na miezi mitatu hajaonekana hadharani.

Akitembelewa mara kwa mara na madaktari, Simone Gbagbo amekua ni mwenye furaha kwa ajili ya siku hii ya kwanza ya kesi hiyo. Mkee huyo wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire anasubiri kuripoti mbele ya majaji ili kujua hasa anachotuhumiwa, mmoja kati ya wanasheria wake amethibitisha. Kwa mujibu wa mwanasheria huyo kesi dhidi ya Simone Gbagbo iko tupu, na haieleweki, kwani hakuna anachotuhumiwa.

Hivi karibuni Mahakama ya kimataifa ya Jinai iliiomba serikali ya Côte d’Ivoire kuikabidhi mkee wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Simone Gbagbo, ili aweze kusikilizwa, lakini serikali ya Cote d'Ivoire ilipinga jambo hilo.

Mahakama ya kimataifa ya Jinai inamtuhumu Simone Gbagbo kuhusika katika machafuko yaliyotokea nchini Côte d’Ivoire baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, machafuko ambayo yalisababisha vifo vya maelfu ya raia.