Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Kijiji cha Bamba chadhibitiwa na makundi yenye silaha

Bemba, pembezoni mwa mto Niger ni kijiji ambacho kinapatikana kwenye umbali wa kilomita 220mashariki ya Timbuktu na kilomita 245  kaskazini magharibi mwa mji wa Gao.
Bemba, pembezoni mwa mto Niger ni kijiji ambacho kinapatikana kwenye umbali wa kilomita 220mashariki ya Timbuktu na kilomita 245 kaskazini magharibi mwa mji wa Gao. Getty Images/Frans Lemmens
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Tangu siku za hivi karibuni, makundi yenye silaha yamekua yakionekana kwa mara nyingine tena katika maeneo ya kaskazini mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Kulikuwa na uporaji, huku milio ya risasi ikisikika katika eneo hilo la kaskazini mwa Mali. lakini wakati huu usalama wa kijiji cha Bamba, kaskazini ya mji wa Gao, unalindwa na makundi mawili ya wanamgambo wa kikabila , ambayo yameyadhibiti maeneo ya mji huo.

Kikiwa kwenye umbali wa kilomita 245 kaskazini mwa mji wa Gao, katika eneo ambapo idadi ya askari ilikua ndogo, kijiji cha Bamba kiko chini ya himaya ya makundi mawili yenye silaha yenye uhusiano wa karibu na serikali ya Mali.

Makundi hayo yaliyotwaa udhibiti wa kijiji cha Bamba ni Gatia pamoja na MAA. Kundi la Gatia lina wanamgambo wengi kutoka jamii ya Watouareg wa Imghad.

Hayo yanajiri wakati ambapo mazungumzo kati ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha yanaanza katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.