KENYA-MWAKA 2015-USALAMA

Rais wa Kenya awahakikishia usalama raia wake

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amewahakikishia raia wake kwamba usalama utaimarishwa katika mwaka 2015. mwaka 2015
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amewahakikishia raia wake kwamba usalama utaimarishwa katika mwaka 2015. mwaka 2015 REUTERS/Presidential Strategic Communications Unit

Nchini Kenya, maelfu walikusanyika katika viwanja vya Jumba la Mikutano ya Kimataifa KICC katikati ya jiji kuupokea mwaka mpya.

Matangazo ya kibiashara

Fataki ziliriushwa hewani katika angaa za jiji la Nairobi kuashiria kuwasili kwa mwaka mpya wa 2015.

Katika hotuba yake ya mwaka mpya, rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa serikali yake itapambana na ugaidi na ufisaidi mwaka huu wa mwaka 2015.

Kiongozi huyo wa Kenya amesisitiza kuwa demokrasioa haiwezi kutumiwa kuwa chanzo cha kuchangia kuwepo kwa utovu wa usalama nchini humo na kuongeza kuwa mwaka 2015 atahakikisha kuwa raia wote wa Kenya wanakua salama.

Hata hivyo raia wengi wa Kenya wanahisi kuwa bado watakabiliwa na tatizo la usalama na maisha kupanda kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwishoni mwa mwaka 2014.