UN-DRC-Dipolmasia-USALAMA

Monusco yashambulia waasi wa Burundi

Helikopta za Monusco zimeendesha mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa kundi la waasi wa Burundi FNL mashariki mwa DRC, Jumatatu, Januari 5 mwaka 2015, alfajiri.
Helikopta za Monusco zimeendesha mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa kundi la waasi wa Burundi FNL mashariki mwa DRC, Jumatatu, Januari 5 mwaka 2015, alfajiri. Photo MONUSCO/Force

Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Monusco kiliendesha jana Jumatatu januari 5 mashambulizi dhidi ya ngome za Kundi la waasi wa Burundi la Fnl katika mkoa wa Kivu Kusini. 

Matangazo ya kibiashara

Monusco imesema mashambulizi hayo hayaendani na tukio liliyotokea hivi karibuni katika wa mkoa Cibitoke, Kaskazini Magharibi mwa Burundi.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametaka kupunguzwa kwa wanajeshi wa kulinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Moon anataka wanajeshi 2,000 kupunguzwa katika kikosi hicho cha wanajeshi elfu ishirini ambacho ndicho kikosi kikubwa cha Umoja wa Mataifa kulinda amani duniani.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa lengo la kupunguza kikosi hicho ni kukiwezesha kufanya kazi yake vizuri.

Jeshi la Monusco liliundwa miaka 15 iliyopita, kuwaondoa waasi hasa Mashariki mwa nchini hiyo na kuhakikisha kuwa inawalinda raia.

Kundi la waasi la FDLR walipewa hadi tarehe mbili mwezi huu kujislaimisha na kuweka silaha chini la si hivyo watakabiliwa kwa nguvu na vikosi vya Umoja wa Mataifa na vile vya DRC.