AFRIKA-CAF-SOKA-AFCON 2015-MICHEZO

Burkina Faso na Equatorial Guinea zatoka sare ya kutofungana

Mchezaji wa Burkina Faso Steeve Yago akikabiliana na mchezaji wa Equatorial Guinea Emilio Nsue Lopez.
Mchezaji wa Burkina Faso Steeve Yago akikabiliana na mchezaji wa Equatorial Guinea Emilio Nsue Lopez. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Timu ya taifa ya Burkina Faso, ambayo ilichukua nafasi ya pili ya mabingwa wa Afrika, imetoka sare ya kutofungana na wenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea Jumatano Janurai 21 katika uwanja wa Bata.

Matangazo ya kibiashara

Burkina Faso kwa sasa iko mbali na kufuzu katika robo fainali, kwani ina alama moja tu katika mechi mbili ambazo imeshaceza katika Kundi A.

Huenda Burkina Faso imeiiaga michuano hiyo ya Kombe la mataifa ya Afrika, ambayo inaingia katika robo fainali, baada ya kutoka sare ya kutofungana na Equatorial Guinea.

Burkina Faso, ambayo ilichukua nafasi ya pili ya mabingwa wa Afrika imeanza kujilaumu, baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kushinda mechi yake dhidi ya Equatorial Guinea.

Burkina Faso ilitawala mpira katika kipindi cha kwanza, na kupoteza nafasi nzuri baada ya wachezaji wake kupoteza mipira walipokua wakifika katika eneo la hatari la lango la Equatorial Guinea.

Katika dakika ya 19 ya mchezo, mchezaji wa Burkina Faso, Alain Traoré alipiga mkwaju, lakini kwa bahati mbaya, mpira uligonga mwamba na kutoka nje ya uwanja. Hata hivyo katika dakika za 29 na 30, Burkina Faso ilipata nafasi nzuri, lakini ilikosa umaliziaji.

Katika kipindi cha pili, Equatorial Guinea walikuja juu, na kutawala mpira katika kipindi chote hicho hadi kipenga cha mwisho.

Kundi A

Naf Timu M Al
1 Gabon 2 4
2 Equatorial Guinea 2 2
3 Congo 2 2
4 Burkina Faso 2 1