Kipengele cha utata chafutwa
Imechapishwa:
Kambi ya wabunge wanaomuunga mkono rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wameupigia kura mswada mwingine wa sheria kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi.
Wakati huohuo kipengele ambacho kilizua utata na kushuhudiwa machafuko juma lililopita katika miji mbalimbali nchini Hamhuri ya kidemokrasia ya Congo kimeondolewa.
Hata hivyo wataalamu na wanadiplomasia wameonya kuwa utulivu nchini humo huenda ukawa wa muda mfupi tu, na kuzua hali ya wasiwasi katika siku zijazo wakati huu maandamano mapya yakitarajiwa kufanyika leo jijini Kinshasa.
Spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Aubin Minaku ndie ambae alitangaza kuondolewa kwa kipengee hicho tata.
Uamuzi huo umefanyika baada ya kushuhudia mauaji ya watu wanaokadiriwa kufikia kati ya 13 na 42 kulingana na duru mbalimbali jijini Kinshasa na miji mingine nchini humo.
Upinzani nchini Congo umekaribisha kuondolea kwa kipengele hicho, huku ukijisifu kuwa umepata ushindi kwa kile ilichokua ikidai.