Wakuu wa mataifa ya AU wakutana Addis Ababa, Waasi wa Ajamhuri ya afrika ya kati wasaini makubaliano ya amani.

Sauti 21:23

Katika makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri Wiki hii, tunaangazia mkutano wa viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa nchini Ethiopia, Upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuitaka tume huru ya uchaguzi nchini humo kutangaza kalenda ya Uchaguzi,Kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, na makundi ya waasi nchini Sudan Kusini juma hili yaliwaachilia huru watoto zaidi ya mia mbili, Marekani kutishia kuiwekea urusi Vikwazo zaidi, iwapo nchi hiii hatiakubali kuacha kuwafadhili waasi wa mashariki mwa Ukraine.Lakini pia uhusiano kati ya Marekani na Cuba kutiwa dosari.Ungana naye Ruben Lukumbuka kusikiliza makala haya.