DRC-MAANDAMANO-SIASA

Maandamano ya upinzani dhidi ya kukamatwa kwa Muyambo

Mwenyekiti wa chama cha mawakili DRC, Jean-Claude Muyambo (akiwa na kipaza sauti)  2007.
Mwenyekiti wa chama cha mawakili DRC, Jean-Claude Muyambo (akiwa na kipaza sauti) 2007. AFP PHOTO / LIONEL HEALING

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umefanya maandamano Jumanne wiki hii mjini Bukavu katika mkoa wa Kivu Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Waaandaaji wa maandamano hayo wamesema lengo la maandamano hayo ni kukemea mbinu za serikali kutaka kuwanyima wapinzani uhuru wao na kujaribu kuwanyamazishakwa kuwafungulia mashitaka mahakamani.

Ni majuma matatu sasa tangu mpinzani Jean Claude Muyambo afunguliwe mashtaka mjini Kinshasa na kujikuta jela kwa tuhuma za uvunjaji wa uaminifu ambapo anadaiwa kuuza mali isiyo yake huku akifahamu vilivyo, tuhuma ambazo hazitambuliki na wanasheria wake.

Mmoja kati ya wanasheria wa Muyambo, Théodore Ngoy amebaini kwamba mtja wake hana hatia, na kesi inayomkabili iko tupu.

" Hakuna kosa la uvunjaji wa uaminifu kwa sababu kosa hilo linaweza kuhusiana na majengo", amesema wakili Ngoy, huku akiongeza kuwa " kulikuwa hakuna ukiukwaji wa mkataba kwa sababu inafaa mmiliki peke yake, atoe malalamiko yake kuwa mali yake Jambo ambalo si kweli hapa. Muyambo hakuuza jumba lolote."