MALI-UFARANSA-UGAIDI-USALAMA

Mali: wanajihadi 12 wauawa

Mwanajeshi wa Ufaransa wa kikosi Barkhane nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014.
Mwanajeshi wa Ufaransa wa kikosi Barkhane nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney

Wanajihadi 12 waliuawa wakati wa operesheni ya majeshi ya Ufaransa Barkhane, usiku wa Januri 30 na 31.

Matangazo ya kibiashara

Opersheni hio iliendeshwa katika eneo la Ifoghas, wizara ya ulinzi ya Ufaransa imefahamisha. Wakati wa operesheni hio, “ magaidi 12 wameuawa” na “ upande wa majeshi ya Ufaransa hakuna hasara iliyotokea”, imesema wizara ya ulinzi ya Ufaransa.

Operesheni hio haikuandaliwa siku nyingi. Kikosi cha wanajeshi ya Ufaransa Barkhane kiliendesha operesheni hio kufuatia taarifa sahihi kiliyopata kuhusu magaidi hao kwenye milima ya Ifoghas karibu na kijiji cha Abeïbara.

Msafara wa magari yaliyokua yakiwabeba wafuasi wa kiongozi wa kijihadi kutoka Mali. Magaidi watu hao wamesambaratishwa, ikimaanisha baadhi waliuawa na wengine walikamatwa ili waweze kutoa taarifa zaidi kuhusu aliko kiongozi wao na taarufa zingine muhimu.

Katika operesheni hio silaha kadhaa zilikamatwa, huku magari waliokuwemo magaidi hayo yalichomwa moto.

Ni pigo kubwa kwa wanajihadi, ambao tangazo rasmi linawaita “ magaidi”.