Nigeria: Boko Haram, tishio kwa uchaguzi na usalama

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (akinyoosha mkono juu) katika mkutano na wafuasi wake katika mji wa Gombe Jumatatu, Februari 2 mwaka2014.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (akinyoosha mkono juu) katika mkutano na wafuasi wake katika mji wa Gombe Jumatatu, Februari 2 mwaka2014. REUTERS/Afolabi Sotunde

Raia wa Nigeria wanatakiwa kushiriki uchaguzi wa urais Februari 14 ili kumchagua au la Goodluck Jonathan kwa muhula wa pili kwenye kiti cha urais, wakati ambapo rais huyo amekua akikosolea kwa kushindwa kukomesha mashambulizi ya Boko Haram tangu alipoingilia madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Wakati uchaguzi huo ukikaribia, Boko Harama imezidisha mashambulizi katika baadhi ya maeneo ya Nigeria, na kudhibiti baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi. Wakati Hata hivyo kulitokea mlipuko Jumatatu wiki hii katika mji wa Gombe ambapo Goodluck Jonathan alikua akiendesha mkutano na wafuasi wake, mara baada ya mkutano huo kumalizika.

Mlipuko huo ulitokea katika kituo cha magari mbele ya uwanja wa mpira, ambapo muda mchache kabla kulikua kukifanyika mkutano kati ya Goodluck Jonathan na wafuasi wake, katika mji wa Gombe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mlipuko huo umetokea mara tu baada ya msafara wa rais kuondoka eneo hilo. Watu wawili wamefariki katika shambulio hilo na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa. Wanawake wawili wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo.

Kwa mujibu wa mashahidi, makumi ya ya vijana waliandamana baadae katika mji wa Gombe dhidi ya Goodluck Jonathan, kwa sababu, kama walivyobaini mashahidi hao, chanzo cha shambulio hilo ni ziara ya rais.

Ni kwa mara ya kwanza kundi la Boko Haram linaendesha shambulio likimlenga rais Goodluck Jonathan. Hii ni hali ya hatari ambayo inamkabili rais Goodluck Jonathan, siku chache kabla ya uchaguzi wa urais.

Boko Haram iliendesha hivi karibuni mashambulizi mengine mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya mji mkuu wa Maiduguri. Hata hivyo Jumapili juma lililopita, Boko Haram iliendesha mashambulizi katika mji mkuu wa jimbo la Borno. Lakini jeshi na vikosi vya kiraia vya ulinzi walifaulu kuwarejesha nyuma wanamgambo wa Boko Haram, baada masaa matatu ya mapigano.

Hayo yakijiri, Chad iliwatuma hivi karibuni majeshi yake nchi Nigeria na Cameroon ili kukabiliana na mashambulizi ya Boko Haram, ambayo yamekithiri.