CAMEROON-NIGERIA-CHAD-BOKO HARAM-Usalama

Watu zaidi ya 70 wauawa Cameroon

Wanajeshi wa Cameroon kutoka kikosi cha kupambana dhidi ya Boko Haram, mwezi Julai, kaskazini mwa Cameroun.
Wanajeshi wa Cameroon kutoka kikosi cha kupambana dhidi ya Boko Haram, mwezi Julai, kaskazini mwa Cameroun. AFP PHOTO / REINNIER KAZE

Watu wasiopungua sabini wameuawa Jumatano waiki hii nchini Cameroun kwenye mpaka na Nigeria katika muktadha wa makabiliano baina ya wapiganaji wa kiislam wa Boko Haram na askari wa Cameroun kwa kushirikiana na wale wa Chad.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo ya mjini Fotokol yanadaiwa kuanzishwa na Boko Haram waliokimbia maeneo ya Gamboru siku ya Jumanne wiki hii baada ya kukabiliana na askari wa Chad na kujaribu kuchukua mji huo.

Askari hao wa Cameroon na Chad wamefaulu kuwatimua wanamgambo hao mjini Fotokol baada ya kupata msaada wa kijeshi wa askari wengine wa Cameroon waliotokea maeneo ya Kousseri, Mora na Kolofata, na askari wa Chad waliopiga kambi mjini Gamboru.

Wanamgambo wa Boko Haram waliingia mjini humo usiku wa jumanne Februari 3 kuamkia Jumatano Februari 4 na kuwaua raia kadhaa, kuchoma moto nyumba na majengo ya serikali ambapo mskiti mkuu wa mjini humo uliteketezwa kwa moto.

Tathmini ya awali inaonyesha kuwa jumla ya askari sita wanaripotiwa kuuawa na huku kukiwepo na miili ya watu takriban sabini ikizagaa mitaani, huku hali ya utulivu ikianza kurejea.