DRC-UN-MVUTANO-DIPLOMASIA

Mvutano waibuka kati ya DRC na UN

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetupilia mbali makataa iliyowekewa na Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange (kushoto), wakipeana mkono katika kikao cha 69 cha Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 25 mwaka 2014
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon (kulia) na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange (kushoto), wakipeana mkono katika kikao cha 69 cha Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 25 mwaka 2014 ©Monusco
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa uliitaka serikali ya Kinshasa kuwafuta kazi maofisa wake wawili wa juu wa jeshi ambao walitajwa kwenye ripoti yake kuwa walihusika na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la M23.

Umoja wa Mataifa, uliipa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, muda wa majuma mawili kwa kuwa shughulikia maafisa hao, na nafasi zao ziwe zimechukuliwa na watu wengine kabla ya tarehe 13 mwezi huu ama vingine vyo umoja huo utaacha kushiriki operesheni za pamoja na jeshi la Serikali.

Katika hatua nyingine, serikali ya Kinshasa imesema kuwa imedhamiria kufungulia mitandao yote ya huduma za kutuma jumbe za simu za mkononi, mwishoni mwa juma hili.

Hata hivyo wanaharakati wa haki za binadamu walikosoa hatua hiyo ya serikali wakisema kuwa haikusaidia kwa lolote katika kuzima maandamano ya kupinga sheria mpya ya uchaguzi, iliyokuwa imepingwa na upinzani wakihofia kuongezewa kwa rais Kabila muda wa kusalia madarakani.