MALI-ALGERIA-WAASI-AMANI-USALAMA

Mali: mchakato wa amani hatarini

Kaskazini mwa Mali kulishuhudiwa umwagaji damu mwishoni mwa juma hili lililopita. Makundi hasimu yenye silaha yalikabiliana kwa mara nyingine tena, karibu na kijiji cha Tessit.

Mazungumzo ya amani kati ya waasi wa kaskazini mwa Mali na serikali yakianzishwa Jumatatu Oktoba 20 mwaka 2014.
Mazungumzo ya amani kati ya waasi wa kaskazini mwa Mali na serikali yakianzishwa Jumatatu Oktoba 20 mwaka 2014. RFI/Leïla Beratto
Matangazo ya kibiashara

Kundi la waasi la MNLA linalishtumu jeshi la Mali kulisaidia kundi la Gatia, lenye ushirikiano na serikali katika vita dhidi yake. Hata hivyo seriklai ya Bamako imekanusha tuhuma hizo.

Hali ya taharuki imeendelea kutanda magharibi mwa kijiji cha Tessit. Hali ya taharuki imeendelea kutanda pia katika jimbo la Tabankort, ambapo makundi ya waasi na makundi yenye silaha yenye mahusiano na serikali ya Bamako yameendelea kujidhatiti.

Jumapili Februari 8, vyanzo vya habari vimeshuhudia makundi hayo yakiendelea kuongeza wapiganaji wao kwenye ngome zao kusini mwa kijiji cha Tabankourt. Kuna uwezekano kutokea kwa mapigano kati ya makundi hayo hasimu, hususan kaskazini mwa Mali.

Katika taarifa iliyotolea jana Jumapili, Umoja wa Mataifa umelani hali hiyo ya wasiwasi na machafuko ambayo, wakati wowote yanaweza kujitokeza mali, na kuzitaka pande husika kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Serikali ya Algeria imekua na imani kuwa amani huenda ikapatikana ndani ya siku 100. Hata hivyo mazungumzo yanaendelea, lakini hakuna matumaini katika mazungumzo hayo.

Rasimu ya mkataba wa amani imekua ikikosolewa na baadhi ya wanasiasa na mashirika ya kiraia nchini Mali. Hata serikali ya Mali imejizuia kueleza chochote kuhusu rasimu hiyo ya mkataba wa amani.