Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Cote d'ivoire yapokelewa kwa vifijo na nderemo

Uwanja wa mpira Felix Houphouët-Boigny, mjini Abidjan, Februari 9 mwaka 2015.
Uwanja wa mpira Felix Houphouët-Boigny, mjini Abidjan, Februari 9 mwaka 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU

Timu ya taifa soka ya Cote d'Ivoire imepokelea kwa vifijo na nderemo katika mji mkuu wa Cote d'Ivoire Jumatatu wikii, ilipowasili kwenye uwanja wa ndege.

Matangazo ya kibiashara

Cote d'Ivoire ilirejea nchini baada ya ushindi wao wa mabao 9 kwa 8 dhidi ya Ghana. Kwa muda wa dakika 120 timu hizo zili kwenda sare ya kutofungana.

Kwa mujibu wa polisi, timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire ilipokelewa na watu milioni moja, ambao walikua kuanzia uwanja wa ndege hadi kwenye uwanja wa mpira wa Félix Houphouët-Boigny. Siku ya jana Jumatatu ilitangazwa kuwa ya mapumziko na italipwa kwa wafanyakazi.

Hervé Renard, kocha wa timu ya taifa soka ya Cote d'Ivoire.
Hervé Renard, kocha wa timu ya taifa soka ya Cote d'Ivoire. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoie Hervé Renard amefurahia kurudi kwake nchini Cote d'Ivoire, huku timu yake ikiwa imepata ushindi.

Renard amebaini kwamba ushindi huu unamkumbusha ushindi wa timu ya taifa ya soka ya Zambia iliyoupata katika mazingira kama haya ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012, wakati alikua kocha wa timu hiyo.

" Nina furaha sana kwa wananchi wote wa Cote d'Ivoire, ambao walisubiri kwa ushindi huu kwa miaka 23. Ujumbe wangu tangu tulipoanza maandalizi Januari 5 ulikua ni ule ule, hata wakati tulianza vibaya kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya Guinea, tulikua hatunaa hofu yoyote, tulikuwa tukiambiana baadhi ya ukweli . Wachezaji walionesha uwezo wao, na matunda yameonekana", Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire alisema, baada ya ushindi wa timu yake.