MALI-ALGERIA-WAASI-USALAMA

Matumaini ya kuendelea kwa mazungumzo ya amani

Waziri Mkuu Modibo Keïta (wa 3 kushoto), aliyekuwa pia mwakilishi wa Mali katika mazungumzo ya amani na makundi ya waasi, atasafiri Jumanne Februari 10 Algiers.
Waziri Mkuu Modibo Keïta (wa 3 kushoto), aliyekuwa pia mwakilishi wa Mali katika mazungumzo ya amani na makundi ya waasi, atasafiri Jumanne Februari 10 Algiers. AFP PHOTO / AHMED OUOBA

Waziri wa mambo ya nje wa Mali, akiwa pia kiongozi wa ujumbe wa Mali kati amazungumzo na waasi, anatazamiwa kuwasili Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, katika kikao kipya cha kuamua kuendekea kwa mazungumzo na makundi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo akiambatana na Waziri wa mawasiliano, alikutana Jumatatu wiki hii na vyombo vya habari.

“ Tunajielekeza Algeria kwa moyo wa matumaini, na vile vile kufuatia ongezeko la hali ya machafuko”, amesema Waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdulaye Diop.

Kuhusu rasimu ya mkataba uliopendekezwa na upatanishi, Waziri wa mambo ya nje wa Mali amesema kuna mafanikio makubwa.

" Waraka huu unazitaka pande husika kuheshimu uhuru wa taifa, kuheshimu taratibu za tabia na muingiliano wa jamii mbalimbali, na vile vile muundo wa serikali moja ya Mali", Waziri Diop ameelezea furaha yake.

Hata hivyo kundi la waasi la Azawad bado linaendelea kushikilia maeneo ya Toumbouctou, Gao na Kidal, huku likibaini kwamba, maeneo hayo ni huru kwa kuunda serikali yake.

Waziri mkuu wa Mali Modibo Keïta, anatazamiwa kujielekeza katika mji mkuu wa Algeria, Algiers ili kuyapa umuhimu mazungumzo hayo na kuonesha nia ya serikali ya Mali ya kutafutia ufumbuzi matatizo yanayoikabili nchi hiyo.