UFARANSA-MOROCCO-DIPLOMASIA

Ufaransa na Morocco zaboresha maridhiano

Mfalme wa Morocco Mohammed wa 6 amepokelewa Jumatatu wiki hii, na François Hollande katika Ikulu ya Elysée.

Mkutano kati ya Francois Hollande na Mohammed wa 6 ambao unasitisha uhasama wa kidiplomasia uliodumu mwaka mmoja kati ya Morocco na Ufaransa, Katika Ikulu ya Elysee, Paris, Februari 9 mwaka 2015.
Mkutano kati ya Francois Hollande na Mohammed wa 6 ambao unasitisha uhasama wa kidiplomasia uliodumu mwaka mmoja kati ya Morocco na Ufaransa, Katika Ikulu ya Elysee, Paris, Februari 9 mwaka 2015. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unafufua mazungumzo kati ya nchi hizo mbili na unasitisha mdororo wa kidiplomasia ambao ulidumu mwaka.

Kuanza kwa mazungumzo hayo kunakuja wakati ambapo jarida la Ufaransa Le Monde limechapisha uchunguzi kuhusu akaunti za kibinafsi za familia ya kifalme nchini Morocco.

Ziara ya mfalme wa Morocco nchini Ufaransa ni muhimu, kwani mahusiano ya kidiplomasia hayakua mazuri kati ya nchi hizi mbili tangu mwezi Februari mwaka 2014, wakati ambapo polisi ya Ufaransa ilimkabidhi hati ya kutafutwa mkuu wa Idara ya ujasusi wa Morocco, Abdellatif Hammouchi, ambaye alikuwa ziarani mjini Paris. Hati ambayo ilitolewa kufuatia ombi la mashirika kadhaa ya Ufaransa, ambayo yakitaka kiongozi huyo afunguliwe mashitaka.

Tangu wakati huo, mdororo wa kidiplomasia uliendelea kushuhudiwa, na hali hiyo iliendelea kushika kasi baada ya Paris na Algiers kuimarisha ushirikiano wao tangu uchaguzi wa François Hollande. Hali hiyo imesababisha kuvunjika kwa uhusiano katika sekta ya sheria kwa miezi kadhaa sasa, na ushirikiano wa kiusalama pia umedorora, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Elysée, Waziri mkuu Manuel Valls na Waziri wa mambo ya nje laurent Fabius wanatazamiwa kujierlekeza nchini Morocco hivi karibuni ili kuendelea na mazungumzo ya kuboresha maridhiano kati ya Ufaransa na Morocco.