MISRI-LIBYA-IS-UGAIDI-MAPIGANO-USALAMA

Misri yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa

Ndege za kivita za Misri ziliendesha mashambulizi Jumatatu, Februari 16 mwaka 2015 dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, nchini Libya, kufuatia kuuawa kwa raia wake 21 wa madhehebu ya Coptic.
Ndege za kivita za Misri ziliendesha mashambulizi Jumatatu, Februari 16 mwaka 2015 dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, nchini Libya, kufuatia kuuawa kwa raia wake 21 wa madhehebu ya Coptic. AFP PHOTO / HO / EGYPTIAN MINISTRY OF DEFENCEAFP PHOTO

Misri imekua kwenye mstari wa mbele wa jumuiya ya kimataifa kwa kuomba Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuingilia kijeshi kimataifa nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiiyo ya Misri inakuja siku moja baada ya kuendesha mashambulizi ya angani katika aridhi ya Libya dhidi ya ngome za kundi la wanamgambo wa kiislamu lenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Doala la Kiislamu, ambalo liliwaua kwa kuwakata vichwa hivi karibuni Wakristo 21 wa madhehebu ya Coptic.

Misri ambayo ni moja ya nchi za Kiarabu yenye nguvu kijeshi, imesema iko tayari kuungana na mataifa mengine kwa kutokomeza ugaidi duniani.

Suala hili ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaotazamiwa kufanyika Jumatano jioni wiki hii. Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Sameh Choukri, atakuwepo katika mkutano huo.

Siku moja baada ya mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na Misri pamoja na Falme za Kiarabu dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu katika mji wa Derna, nchini Libya, serikali ya Mirsi, ambayo inatiwa wasiwasi na mashambulizi ya kundi la kiislamu lenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu katika eneo la Sinai, imeomba Umoja wa Mataifa kuiunga mkono katika vita inayoendesha katika mpaka wake, mashariki na Libya.

Rais wa Misri, Abdel Fatah al Sisi, ameomba Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kukipa uwezo kikosi cha Umoja wa Mataifa kuingilia kijeshi nchini Libya. Kwa upande wake Italia, ambayo ilitawala Libya katika enzi za ukoloni, imependekeza kutuma wanajeshi 5000 nchini humo. Ufaransa, ambayo iliomba mara kadhaa, kupitia Waziri wake wa ulinzi, kuingilia kijeshi nchini Libya, imeomba mkutano huo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuchukua hatua mpya dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, kwa mujibu wa tangazo la Ikulu ya Elysée.