BURUNDI-MAPIGANO-USALAMA

Rais Nkurunziza amfuta kazi mkuu wa Idara ya ujasusi

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amfuta kazi mkuu wa Idara ya ujasusi, baada ya kumsihi kutogombea muhula watatu.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amfuta kazi mkuu wa Idara ya ujasusi, baada ya kumsihi kutogombea muhula watatu. AFP PHOTO/Brendan SMIALOWSKI

Hivi karibuni mkuu wa Idara ya ujasusi, jenerali Godefroid Niyombare alimuandikia Rais wa Burundi akimsihi kutogombea muhula watatu, kwa kuhofia kuitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko, kwa mujibu wa vyanzo viliyo karibu na jenerali huyo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya madai hayo kukanushwa na watu walio karibu na Rais Pierre Nkurunziza. Hata hivyo Rais huyo amechukua uamzi Jumatano jiono wiki hii wa kumfuta kazi mkuu huyo wa Idara ya ujasusi.

Hayo yanajiri wakati ambapo mgawanyiko umejitokea katika chama tawala cha Cndd-Fdd kuhusu kugombea kwa Rais Pierre Nkurunziza muhula watatu. Hivi karibuni Seneta kutoka chama cha Cndd-Fdd, Richard Nimbesha alitoa msimamo wake kuhusu kugombea kwa Pierre Nkurunziza kwa muhula watatu.

Seneta Richard Nimbesha, alipinga kugomea kwa rais Nkurunziza kwa muhula watatu, jambo ambalo lilisababisha mgawanyiko katika chama hicho.

Rais Nkurunziza amewafuta kazi pia maafisa wengine waandamizi wa Idara ya ujasusi, ikiwa ni pamoja na mkuu wa itifaki kwenye idara hiyo, Léonard Ngendakumana, pamoja na mkuu wa usalama wa ndani kwenye Idara hiyo, Ndayizeye Sylvestre Abdallah.

Jenerali Godefroid Niyombare alikua aliteuliwa hivi karibuni katika wadhifa huo, baada ya miezi kadhaa kuteuliwa kuwa balozi wa Burundi nchini Kenya.

Jenerali, Godefroid Niyombare alikua mkuu wa majeshi ya Burundi kwa zaidi ya miaka mitatu, kabla ya kufutwa kazi na kuteuliwa kuwa balozi nchini Kenya. Mpaka sasa jina la aliyemrudilia halijafahamika.