BURUNDI-MAANDAMANO-RPA-SIASA

Maandamano, onyo kwa Nkurunziza

Umati wa watu mbele ya makao makuu ya redio RPA, Alhamisi Februari 19 mwaka 2015, Bujumbura, Burundi.
Umati wa watu mbele ya makao makuu ya redio RPA, Alhamisi Februari 19 mwaka 2015, Bujumbura, Burundi. AFP PHOTO/Esdras NDIKUMANA

Uhamasishaji haukua wa kawaida, Alhamisi, Februari 19, katika mitaa ya mji wa bujumbura, nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya raia waliandamana kufuatia tukio la kuaciliwa huru kwa mkurugenzi wa redio RPA, Bob Rugurika, baada ya kuzuiliwa jela kwa mwezi mmoja.

Alipowasili katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, Bob Rugurika, alipokelewa na mamia kwa maelfu ya raia ambao walimiinika mitaani na kudhihirisha furaha yao.

Hayo yanatokea ikisalia miezi mitatu tu kabla ya uchaguzi wa kwanza kwa jumla ya chaguzi nne zitakazofanyika mwaka huu nchini humo.

Raia walishiriki maandamano bila ruhusa ya serikali, wakati ambapo maandamano ya aina yoyote yalikua yalipigwa marufuku na utawala.

Maandamano ya Jumatano na Alhamisi wiki hii mjini Bujumbura ni ishara muhimu kwa utawala wa Pierre Nkurunziza.

Ni kwa mara ya kwanza watu zaidi ya elfu 6 kumiminika mitaani katika mji wa Bujumbura tangu nchi hii iingiye katika mfumo wa vyama vingi.

Wadadisi wanasema maandamano hayo ni ishara kuwa raia wamechoshwa na utawala, na wanataka mabadiliko.