Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Viongozi wa mataifa ya afrika mashariki wakutana jijini Nairobi, Raisi wa Tanzania akabidhiwa Uongozi wa EAC

Imechapishwa:

Viongozi wa mataifa matano wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki wamekutana juma hili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.Katika kikao hicho Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alipokezwa uenyekiti wa Jumuiya hiyo baada ya Uhuru Kenyatta wa Kenya.Mustakabali wa mataifa ya Somali na Sudan Kusini pia yalijadiliwa.Na huko DRC, jeshi la umoja wa mataifa Monusco limesusia kushiriki mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kundi la FDLR.Kimataifa rais wa Marekani alisema yuko tayari kuhamasisha umoja wa mataifa yote ili kudhibiti ugaidi na kuainisha msimamo kwamba marekani haiko dhidi ya Uisilamu.Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza makala haya.  

Sayari ya dunia
Sayari ya dunia