COTE D'IVOIRE-SIMONE-SHERIA

Simone Gbagbo: “ Gbagbo alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2010"

Katika utetezi wake mbele ya majaji, baada ya kuonekana hadharani tangu alipokamatwa mwezi Aprili mwaka 2011, Simone Gbagbo amekanusha tuhuma dhidi yake, huku akibaini kwamba “Laurent Gbagbo ni mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2010”.

Simone Gbagbo à son arrivée à la cour d'assises d'Abidjan, lundi 23 février 2015.
Simone Gbagbo à son arrivée à la cour d'assises d'Abidjan, lundi 23 février 2015. AFP/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Simone Gbagbo anatuhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa. Uhalifu uliyotekelezwa wakati wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi, kati ya miaka ya 2010 na 2011. Machafuko ambayo yaligharimu maisha ya watu takribani 3000 kutoka pande zote zilizokua zikihasimiana.

Baada ya kusikilizwa kwa mawaziri kadhaa katika utawala wa Laurent Gbagbo pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa viliyokua vikishirikiana na utawala wakati huo majuma kadhaa yaliyopita, hatimaye Simone Gbagbo amesikilizwa na vyombo vya sheria vya Côte d’Ivoire.

Awali mmoja kati ya wanasheria wa Simone Gbagbo, Habiba Touré, amewasihi baadhi ya watu ambao wamekua wakithibitisha kwamba mteja wao alihusika katika machafuko yaliotokea katika miaka ya 2010 na 2011 nchini Côte d’Ivoire.

“ Unaweza ukasema kuwa hauhusiki katika makosa unayotuhumiwa bila hata hivyo kufanya vitisho. Kwa hiyo Simone Gbagbo ataweka wazi ukweli wake. Na upande wa mashitaka utatoa ushahidi wake”, amesema Habiba Touré