Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-ETHIOPIA-MAZUNGUMZO-Usalama-SIASA

Wahusika muhimu wakosekana katika mazungumzo

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini  na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Goran Tomasevic
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudani Kusini yalianza tena Jumatau Februari 23 mjini Addis Ababa, Ethiopia, lakini rais wa Sudani kusini Salva Kiir na makamo wake wa zamani, Riek Machar hawakuwepo katika mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo imejitokeza wakati kikao hiki cha mazungumzo kinachukuliwa na wasuluhishi kutoka Afrika Mashariki kuwa ni mazungumzo ya bahati ya mwisho, baada ya mwaka mmoja, pande zinazohasimiana kushindwa kufikia muafaka.

Rais Salva Kiir na hasimu wake, Riek Macgar waliahidi kuwepo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha mazungumzo, lakini hawakuwasili.

Kiongozi kamati ya usuluhishi kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika ya Mashariki Igad, Seyoum Mesfin, ameonya kuwa mazungumzo haya ni bahati ya mwisho ambayo imepewa viongozi wa Sudani kusini kwa kuweza kufikia mkataba.

“ Mazungumzo haya ni ya mwisho. Ni bahati ya mwisho ya kuendelea kwenye karne ya amani nchini Sudani Kusini. Hutupaswi kushindwa, tunapaswa kuhakikisha kuwa mkataba umefikiwa”, amesema Seyoum Mesfin.

Ujumbe kutoka pande hizo mbili wana siku 15 hadi Machi 5 ili wawe wameafikiana kuhusu kugawana madaraka kati ya Salva Kiir na Riek Machar katika serikali ya mpito. Wanadiplomasia wameeleza kwamba kamati ya usuluhishi inataka pande husika katika mgogoro unaoendelea kufikia kwenye mkataba wa kudumu, lakini hakuna ishara yoyote ambayo inaonyesha kuwa mkataba huo utatekelezwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.