Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-KIIR-MACHAR-MAZUNGUMZO-USALAMA

Serikali ya mpito bado inasubiriwa Sudan Kusini

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini  bado anasubiriwa katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini bado anasubiriwa katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Goran Tomasevic
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mkutano muhimu uliotarajiwa kati ya Rais wa Sudan Kusini na Kiongozi wa waasi Riek Machar, umegonga mwamba baada ya  Kiir kuchelewa kujielekeza  mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako mpinzani wake Machar amewasili.

Matangazo ya kibiashara

Kutoonekana kwa Kiir kwenye mkutano huo kumegadhabisha  Kitengo cha kulinda Usalama cha Umoja wa Mataifa ambacho kinatarajiwa kuiwekea  serikali ya Sudan Kusini vikwazo vikali.

Hayo yakiendelea, mjini Juba, Rais Salva Kiir ameamuru vikosi vyake vikomeshe mapigano na waasi na pia amewaita nyumbani wanasiasa kumi  walioko uhamishoni na ambao  aliwasamehe baada ya kudai kuwa walipanga njama za kuipindua serikali yake mwezi Desemba mwaka 2013.

Kukiwa kumebaki  siku saba ili Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar waanzishe rasmi serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa, wingu la kutatanisha lbado limetanda mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako wawili hao walitarajiwa kukutana kuweka sahihi kwenye makubaliano ya mwisho na ya amani ya kudumu.

Tayari Kiongozi wa waasi Riek Machar amewasili Addis Ababa, lakini Rais Salva Kiir ambaye wapatanishi wa IGAD wamemsubiri, hajawasili Addis Ababa na inasemekana kuwa bado angali Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Kinachoendelea kwenye sehemu ya mkutano ni majadiliano ya kina kati ya makundi yanayowawakilisha Rais Kiir na Machar.

Kufikia jioni hii ya Alhamisi, wawakilishi hao wamepitia kwa makini vipengele mbalimbali vinavyohusika na kuleta amani. Wanadiplomasia  wanaohudhuria mkutano huo wanaarifu kuwa wawakilishi hao wameshindwa kukubaliana kuunganisha vikosi vya serikali na vya waasi katika  serikali ya muungano.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.