MALI-ALGERIA-WAASI-AMANI-USALAMA

Mkataba wa amani Mali wasusiwa na CMA

Bilal Ag Acherif, mwakilishi wa MNLA, wakati wa sherehe ya kuhitimisha mazungumzo kati ya raia wa Mali mjini Algiers, Machi 1 mwaka 2015.
Bilal Ag Acherif, mwakilishi wa MNLA, wakati wa sherehe ya kuhitimisha mazungumzo kati ya raia wa Mali mjini Algiers, Machi 1 mwaka 2015. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE

Rasimu ya mkataba wa amani nchini Mali, haikusahihishwa na baadhi ya makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi hio. Muungano wa makundi yenye silaha ya Azawad (CMA) umeomba muda wa kutafakari kabla ya kutoa msimamo wao.  

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake serikali na makundi mengine yenye silaha yanayounga mkono serikali ya Mali, wammesahihisha mkataba huo ulioandaliwa na timu ya usuluhishi. Sherehe za kutia sani kwenye mkataba huo zimepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Machi mjini Bamako, nchini Mali.

Kulingana na taarifa ambazo RFI imepata, muungano wa makundi yenye silaha (MCA) utatoa uamzi wake tarehe 10 Machi mwaka 2015.

Mkataba huo umesahihishwa kufuatia miezi saba ya mazungumzo yenye lengo la kukomesha mvutano wa kisiasa kaskazini mwa Mali. Hata hivyo mkataba huo haukuridhisha makundi yote hasimu, hususan yale yanayoomba kujitegemea kwa maeneo wanaoshikilia. Mkataba huo umetiliawa saini na pande zote husika, ispokua muungano wa makundi ya waasi ya Azawad (CMA).

Jumapili Machi 1, mkataba wa amani na maradhiano kuhusu Mali umesahihishwa na serikali ya Bamako pamoja na baadhi ya makundi yenye silaha yaliowakilishwa katika mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. Hata hivyo muungano wa makundi yenye silaha ya Azawad (CMA), unaoundwa na MNLA, Baraza kuu la umoja wa Azawad, MAA pamoja na CPA umeeleza kwamba muda haujawadia wa kusahihisha mkataba huo.

Msemaji wa ujumbe wa muungano wa CMA katika mkutano wa Algiers, Mohamed Ousmane, ameeleza kwamba hawajakataa kutia saini kwenye mkataba huo, bali ni suala tu la muda.

“ Tumesema kua mkataba waliopendekeza ni moja ya mikaba bora tulioshuhudia kwa kutanzua migogoro kati yetu”, amesema Mohamed Ousmane.

Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya, akiwa pia Mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Mali, amebaini mbele ya wajumbe wa muungano huo wa makundi yenye silaha ya CMA kwamba bado milango iko wazi kwa makundi hayo.

“ Tuna imani na nyinyi, na tunafahamu kwamba mko kwa amani ya taifa la Mali”, amesema Pierre Buyoya Jumapili asubuhi Machi 1, huku akibaini kwamba hana hofu, ndani ya siku kadhaa makundi hayo yatasahihisha mkataba wa amani na maridhiano ulitiliwa saini na makundi mengine pamoja na serikali ya Bamako.