RWANDA-UFARANSA-DIPLOMASIA

Paul Kagame akutana na Nicolas Sarkozy Paris

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame. DR

Kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya Ikulu ya Rwanda, rais Paul Kagame amekutana Ijumaa Februari 27 mjini Paris na rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy. Washirika wa karibu wa Nicolas sarkozi wamethibitisha mkutano huo kati ya wawili ho.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Paul Kagame hakukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Rais wa Rwanda alikua alijelekeza Ufaransa kushiriki katika mkutano kuhusu intaneti kwa mwaliko wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya sayansi na utamaduni Unesco, ambapo ni mmoja kati ya viongozi wa hamashauri ya intaneti.

Ikulu ya Rwanda ndio ilianza kufahamisha kupitia akaunti yake ya Twuiter kuhusu mkutano huo kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

Kwa mujibu wa idara ya habari ya kiongozi wa chama cha UMP, mkutano huo ulifanyika Ijumaa mchana wiki hii kwa jitihada za rais wa Rwanda, katika hoteli alikofikia Paul Kagame. Hakuna maelezo kuhusu undani wa mazungo ya wawili hao. Washirika wa karibu wa Nicolas Sarkozy wamebaini kwamba, wakati wa utawala wake, Nicolas Sarkozy alikua alijenga na kuboresha uhusiano wa imani na rais wa Rwanda.

Mkutano huo kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, umefanyika wakati uhusiano kati ya nchi hizi mbili umekua si mzuri wakati huu. Mwaka uliopita, rais wa Rwanda Paul Kagame aliituhumu Ufaransa kuwa ilishiriki moja kwa moja katika mauaji ya kimbari yaliotokea mwaka 1994.

Tangu wakati huo, kulifanyika mkutano mmoja tu kati ya afisa mwandamizi wa Ufaransa na Paul Kagame.

Hivi karibuni Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius alimuomba rais Paul Kagame mjini Libreville, nchini Gabon kutoa maelezo zaidi kuhusu kushiriki kwa Ufaransa katika mauaji ya kimbari yaliotokea nchini humo mwaka 1994. Paul kagame, aliahidi wakati huo kuwa atamtumia barua rais wa Ufaransa, François Hollande. Ufaransa imebaini kwamba haijapokea barua hio tangu wakati rais Paul Kagame alipotamka maneno hayo.

Hata hivyo kwenye televisheni France 24, rais Paul kagame amebaini kwamba hajawa na uhasama na Ufaransa, na angelifurahishwa kujielekeza nchini Ufaransa kwa wakati wowote, amesema Kagame,