LIBYA-IS-Uteuzi-Siasa-Usalama

Jenerali Haftar ateuliwa kuwa kamanda mkuu wa jeshi

Viongozi wa Tobrouk, ambao wanatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, wamemteuwa Jumatatu wiki hii jenerali Haftar kuwa kamanda mkuu wa jeshi lao. Uteuzi huu umeweka matatani hali inayojiri wakati huu nchini Libya.

Jeneral Khalifa Haftar katika mji wa Abyar, mashariki ya Benghazi, Mei 31 mwaka 2014.
Jeneral Khalifa Haftar katika mji wa Abyar, mashariki ya Benghazi, Mei 31 mwaka 2014. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Tobrouk, ambao wanatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, wamemteuwa Jumatatu wiki hii jenerali Haftar kuwa kamanda mkuu wa jeshi lao. Uteuzi huu umeweka matatani hali inayojiri wakati huu nchini Libya.

Khalifa Haftar amekua kiongozi wa majeshi ya serikali ya Tobrouk tangu mwaka mmoja uliyopita. Jenerali Khalifa Haftar ndiye alianzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa makundi ya kiislamu katika mji wa Benghazi.

Jenerali Khalifa Haftar alihudumu katika jeshi wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Libya Moammar Kadhafi

Jumuiya ya kimataifa haijawahi kumhukumu wala kumuunga mkono hadharani jenerali Haftar nchini Libya.

Mwezi Mei, wakati jenerali huyu alipoanzisha operesheni alioiita “Operesheni ya kiutu”, akimaanisha “ kutokomeza ugaidi”, Marekani iliona kuwa ni shambulio dhidi ya makundi hasimu yenye lengo moja. Baada ya mamia ya watu kuuawa na eneo moja la Benghazi kutekwa, mapigano yameendelea kushuhudiwa hadi leo.

Kundi la Ansar Al Shariah, lenye mafungamano na Al Qaeda, ambalo liliwekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi ni moja ya makundi yanayopigana katika mji wa Bengahzi na maeneo mengine nchini Libya.

Kundi hilo lilihusika pia katika shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani Septemba 11 mwaka 2012 na kuhusika pia katika kifo cha balozi Chris Stevens.