NIGERIA, BOKO HARAM-IS-CHAD-UCHAGUZI-USALAMA

Boko Haram yatumia mbinu za IS kwa kueneza sera zake

Fuvu la mpiganaji wa Boko Haram aliyeuawa katika mlipuko akiwa katika gari lake lisilopitisha risase katika kambi ya Amchidé.
Fuvu la mpiganaji wa Boko Haram aliyeuawa katika mlipuko akiwa katika gari lake lisilopitisha risase katika kambi ya Amchidé. RFI/OR

Kwa kipindi cha miezi miwili Boko Haram imekua ikitumia mbinu zinazotumiwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu nchini Syria na Iraq kwa kupeperusha vitendo viovu inavyotekeleza kupitia mitandao mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa Boko Haram imeanza kujieleza na kueneza ujumbe wake katika lugha ya Kifaransa.

Moja ya njia mbadala ya kuenzea sera zake ni video ambazo zilikua zikitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu. Kwa sasa Boko Haram imekua ikieneza ujumbe wake kupitia Intaneti na Twitter, huku ikiwa na Idara rasmi inayohusika na masuala ya vyombo vya habari.

 

Wafadhili wa Nigeria wameendelea kuipongeza Nigeria kuongeza juhudi kwa kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi wa urais, ambao umepangwa kufanyika Machi 28 mwaka huu, chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya mataifa yanayochangia ziwa Chad.

Kwa ujumla, uchaguzi nchini Nigeria, mara nyingi hugubikwa na vurugu. Mapigano yaliyozuka katika uchaguzi uliopita mwaka 2011 yalisababisha maelfu ya watu kuuuawa. Mohamed Ibn Champas, mwakilishi maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda Afrika Magharibi amevitaka vikosi vya nchi zinazoendesha vita dhidi ya Boko Haram, kuhakikisha kuwa usalama umeimarishwa nchini Nigeria wakati wa uchaguzi.

 

Umoja wa Mataifa unapendelea kikiosi hiki cha kimataifa kinachoendesha vita dhidi ya Boko Haram kiwe na wajibu wa kukabiliana vilivyo na kundi la Boko haram.

Kwa sasa jeshi la Chad linaendesha shughuli zake Nigeria, tofauti na jeshi la Cameroon. Kutokana na hali hio, Umoja wa Mataifa unatazamia kutathmini mwezi Aprili azimio kuhusu kikosi hiki cha kimataifa ili kiweze kupewa msaada wa kifedha na vifaa vya kijeshi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.