DRC-ITURI-ICC-LUBANGA-FIDIA-SHERIA

Waathirika wa Thomas Lubanga watafidiwa

Watu walioathirika katika vita viliyoongozwa na kiongozi wa kivita Thoma Lubanga, ambaye alipatikana na hatia ya kusajili watoto wenye umri wa miaka 15, na kuwatumia katika vita, watapewa fidia.

Thomas Lubanga, akisikilizwa kwenye Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Thomas Lubanga, akisikilizwa kwenye Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo umechukuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC. Thomas Lubanga alihukumiwa mwaka 2012 kifungo cha miaka 14 jela, na kwa sawa ametimiza miaka zaidi ya 7 akiwa kizuizini Hague.

Hukumu ya Thomas Lubanga ilithibitishwa katika Mahakama ya Rufaa Desemba 1 mwaka 2014.

Watu 129 walioathirika katika vita hivyo, walihuzuria kesi dhidi ya mwanamgambo Thomas Lubanga. Wote hao watanufaika na fidia, itakayotolewa na Lubanga. Si hao tu peke yao. Waathiriwa wengine ambao hawakuhuzuria kesi hio mjini Hague, pamoja na familia zao na jamii zao asilia watanufaika pia kwa kufidiwa.

Kwa upande wa waathiriwa katika jimbo la Ituri katika ya mwaka 2002 na 2003 wamesema ni ushindi ambao wamepata baada ya miaka 10 wakisubiri.

Hayo yakijiri vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumapili wiki hii, vimekabidhi mapendekezo yao ya kuboresha kalenda ya uchaguzi kwenye ofisi ya Tume huru ya uchaguzi nchini humo CENI.

Kulingana na vyama hivyo, kalenda ya uchaguzi kama ilivyopendekezwa na Tume Huru ya Uchaguzi haikuchukua maoni ya vyama vya upinzani.

Hata hivyo, serikali ya Congo kwa upande wake inaamini kuwa Tume ina wajumbe kutoka vyama hivyo na kwamba kalenda hiyo imezingatia maoni si tu ya upande wa serikali lakini pia ya vyama vya upinzani.