DRC-AU-UCHAGUZI-USALAMA

DRC : AU yaitaka Ceni kutoshawishiwa na wanasiasa

Tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na maswala ya Uchaguzi imeiomba Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Ceni, kutekeleza kalenda yake ya uchaguzi bila ya kukubali vitisho vya wanasiasa.

Maandamano dhidi ya kupitishwa muswada wa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015.
Maandamano dhidi ya kupitishwa muswada wa sheria mpya ya uchaguzi, katika mji wa Kinshasa, Januari 19 mwaka 2015. AFP PHOTO/ PAPY MULONGO
Matangazo ya kibiashara

Wito huo umetolewa jijini Kinshasa wakati wa warsha ya kubadilishana taarifa kuhusu mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Tume hiyo imependekeza Ceni, kuheshimu kalenda yake iliyotangazwa tarehe 12 mwezi Februari mwaka huu na kutotisjiwa na wanasiasa.

Aidha, mwenyekiti wa jukwaa hilo, Simaro Ngongo, ameiomba Ceni, kutokubali vitisho kutoka kwa wanasiasa wa upande wowote, pamoja na kupokea maoni ya wadau wengine ikiwa yatasaidia kuboresha kazi ya Tume hiyo.

Juma hili, vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong, Ceni, viliwasilisha kwenye Tume huru ya Uchaguzi mapendekezo ya marekebisho ya Kalenda hiyo kwa kile walichokisema kalenda iliyowalishwa haikuwarishikisha wadau wote.